idadi jumla ya watu waliotazama hadithi kufikia sasa
15,942,112

Kurasa zifuatazo ni muhtasari wa hadithi ya kweli. Ni kama hadithi nyingi nzuri ambazo umesikia au kusoma, lakini kadiri unavyosoma zaidi, ndivyo utagundua kuwa hii si hadithi nyingine tu--ni Hadithi ya KIPEKEE. Inatufafanua sisi sote. Inatufanya tufikirie kuhusu utambulisho wetu na kile tunachoweza kuwa. Na hivyo...

mungu

Hadithi inaanza na Mungu, ambaye alikuwepo tangu mwanzo. Amekuwepo tangu mwanzo, na amekuwepo siku zote kama alivyo sasa. Ikiwa inaonekana kutatanisha, ni kwa sababu Yeye ni zaidi ya kile ambacho mtu yeyote anaweza kuelewa kikamilifu.

Mwanzo 1:1 Isaya 40:28

uumbaji

Hapo mwanzo, Mungu alinena na kila kitu kikawepo. Kwa amri Yake, ulimwengu wote mzima uliumbwa na kujazwa na maonyesho makubwa ya galaksi, nyota, na sayari—ikiwemo Dunia, ambako palikuwa na bustani nzuri ya paradiso iitwayo Edeni. Kati ya vitu vyote vizuri alivyoumba, kazi bora zaidi ilikuwa mwanaume na mwanamke. Mungu aliwaumba Adamu na Eva kwa mfano wake ili wafanane na Yeye. Waliumbwa na kusudi kuu la kumwabudu kwa kumpenda, kumtumikia, na kufurahia uhusiano Naye.

Zaburi 8:3 Isaya 40:26

upatano

Kwa mpango wa Mungu, uumbaji wote ulikuwa katika upatano na ulikuwa jinsi ulivyopaswa kuwa. Wakati huu hakukuwa na maumivu, mateso, ugonjwa au mauti. Kulikuwa na upendo kamili, kukubalika, na urafiki kati ya Mungu na binadamu, kati ya Adamu na Eva, na katika uumbaji wote. Lakini kitu cha kusikitisha kilitokea...

Mwanzo 1:31

kutotii

Adamu na Eva hawakuwa sawa na Mungu kwa vyovyote vile, lakini kwa upendo aliwaweka kusimamia vitu vyote alivyokuwa ameviumba katika bustani ya Edeni. Aliwapa uhuru wa kufanya maamuzi na kutawala dunia na kuwapa kanuni moja: kutokula matunda ya mti mahususi. Siku moja, adui wa Mungu, malaika aliyeanguka aitwaye Shetani, alitaka kumpindua Mungu hivyo alichukua mfano wa nyoka na akawadanganya Adamu na Eva. Aliwahadaa wafikiri kuwa Mungu hakuwa mwema na hakuwajali. Kutokana na haya, walikosa kumtii Mungu kwa kujua. Kwa uasi, Adamu na Eva walikula tunda hilo, wakiamua kuwa wao, si Mungu, ndio wangeamua mema na mabaya.

Mwanzo 3:1-6 Warumi 3:23

matokeo

Matokeo ya matendo yao yalikuwa mabaya sana! Kama virusi, dhambi iliingia katika uumbaji wote na ndani ya mioyo ya Adamu na Eva. Dhambi, mateso, na maumivu yalipitishwa kutoka kizazi hadi kizazi; uumbaji wote ulipotoshwa kutoka kwa muundo wake asili. Sote tumesoma au kusikia hadithi za vita, umaskini, magonjwa, tamaa, na kashfa zinazoikumba dunia yetu leo. Hizo zote ni matokeo ya dhambi.

Mwanzo 3:7-8 Isaya 53:6

hitaji

Tunapofikiri kuhusu ukamilifu na upendo uliokuwako mwanzoni mwa uumbaji, tunatambua kuwa “tuna kasoro nyingi na wenye dhambi zaidi kuliko tunavyoweza kuthubutu kuwazia.” Hebu fikiria kuhusu chuki ambazo tumeshikilia, uwongo ambao tumesema, mawazo ambayo hatuwezi kamwe kuthubutu kusema kwa sauti. Mtazamo wa uaminifu ndani ya mioyo yetu wenyewe unaonyesha ukweli: Sisi sote tuna hatia. Kila mtu amefanya dhambi, na matokeo ya mwisho, ambayo ni mbaya zaidi kuliko kifo cha kimwili, ni kutengwa milele na Mungu mwenye upendo, katika taabu mbaya na kutokuwa na furaha. Kutokana na haya yote, tunahitaji kufikiria kuhusu maswali haya: Je, kuna jambo lolote ambalo linaweza kufanywa? Je, kuna tumaini lolote?

Warumi 3:10 Warumi 5:12

ahadi iliyotolewa

Mungu aliwaondoa Adamu na Eva kutoka Edeni kutokana na dhambi yao lakini akawaacha na ahadi ya wokovu na tumaini. Aliwaahidi kuwa mmoja wa wazao wao siku moja angewakomboa binadamu kutoka kwenye dhambi. Katika karne zilizofuata, Mungu alitayarisha njia kwa ajili ya mtu huyu ambaye angekuwa Mwokozi wa ulimwengu. Maelezo kamili ya kuzaliwa Kwake, maisha, na kifo chake yaliandikwa katika Biblia karne nyingi kabla ya kuja Kwake. Hakika, Biblia nzima kimsingi inaonyesha mtu huyu mmoja kama kitovu cha historia yote ya binadamu. Kusudi lake la kuja lilikuwa “kutafuta na kuokoa kile kilichopotea” (Luka 19:10). Kwa hivyo, je, Yeye alikuwa nani?

Isaya 7:14 Isaya 9:6

ahadi iliyotimizwa

Mwokozi aliyeahidiwa, bila shaka, alikuwa Mungu. Mungu alifanyika mwanadamu katika utu wa Yesu Kristo takriban miaka 2,000 iliyopita, akitimiza utabiri wote katika Agano la Kale. Kuzaliwa kwa Yesu kulikuwa tukio la kimuujiza kwani mama yake alikuwa bikira. Maisha yake yalikuwa ya kipekee: Alimfurahia na kumtii Mungu kikamilifu bila kufanya dhambi. Hatimaye hii ilisababisha kifo Chake cha uchungu msalabani kwani kwa hiari, kwa utiifu, na kwa njia ya kutosha alilipia dhambi za binadamu, kulingana na mpango wa Mungu. Katika dhihirisho kuu la rehema na neema ambayo ulimwengu umewahi kujua, maisha na kifo cha Yesu kilichukua nafasi ya wote ambao wangemtumaini. Mtu asiye na hatia kabisa alikufa ili kuwaokoa wenye hatia wasio na tumaini kutoka kwa dhambi na Shetani.

Lakini nguvu za mauti hazikuweza kumshikilia Yesu. Siku tatu baadaye, Yesu alitoka kwenye kaburi Lake, akitimiza dhamira Yake ya duniani ya kuishinda dhambi kwa kufa msalabani na kushinda kifo kwa kufufuka kutoka kwa wafu—kama vile Mungu alivyoahidi. Siku arobaini baadaye alirudi Mbinguni ambako anatawala kama Mfalme halali.

Lakini hadithi haiishii hapo...

Wakolosai 1:13 1 Petro 3:18

Mambo Yote ni Mapya

Kwa wale wote wanaomtumaini Yesu pekee, Mungu ameahidi pia kuwa atafanya mambo yote kuwa mapya. Mbingu mpya na dunia mpya hazitakuwa na dhambi na ubinafsi—mahali pa urafiki kamilifu na Mungu, watu wengine na viumbe vyote. Hapatakuwepo na mitetemeko ya ardhi yenye kuleta uharibifu, tsunami zenye kuharibu au dhoruba kali hazitaikumba dunia. Hapatakuwepo na maumivu, mioyo iliyovunjika, magonjwa au kifo.

Kila kitu kitarejeshwa kuwa jinsi kilivyokusudiwa kuwa. Dunia mpya itakuwa tena makao kamili ambayo Mungu alikusudia kwa uumbaji Wake. Kusudi asili la Mungu litatimia, kwa kuwa wale wanaoamini wokovu Wake wataingia katika kusudi kuu la kumwabudu kwa kumpenda, kumtumikia, na kufurahia uhusiano pamoja Naye milele.

Ufunuo 21:4

Tutakuwa na Mungu Milele

Sehemu nzuri zaidi ya ulimwengu huu mpya ni kuwa tutakuwa pamoja na Mungu milele, tukiwa na furaha kamili. Tutarejeshwa kwenye uhusiano mkamilifu na Yule aliyetuumba, aliyetupenda, na kufa kwa ajili yetu. C. S. Lewis, msomi na mwandishi wa vitabu vya watoto, alilinganisha hatua ya kwanza katika ulimwengu huu mpya kama “Sura ya Kwanza ya Hadithi Kuu ambayo hakuna mtu duniani ambaye amewahi kuisoma: ambayo inaendelea milele: ambayo kila sura ni bora zaidi kuliko ile iliyotangulia.

Ufunuo 22:3-5 II Wakorintho 5:8

Je, sehemu yako katika hadithi ni gani?

Mungu anaandika hadithi nzuri mno kutoka kwa uumbaji hadi urejesho. Alikuumba uwe sehemu ya hadithi hiyo ili umwabudu, umtumikie, na kufurahia uhusiano Naye. Kwa kujiunga na Mungu katika hadithi Yake, utapata msamaha, kusudi, na kuridhika unapomjua Mwanzilishi wa maisha.

Mathayo 11:28-29

Wokovu kwa Imani Pekee

Imani ni tumaini rahisi katika Yesu Kristo pekee kukuokoa. Inamaanisha kuwa badala ya kuamini kuwa unaweza kujiokoa kutokana na matokeo ya dhambi, unaweka imani yako kwenye uokoaji aliokununulia kwa kifo chake. Imani yako sasa iko kwa Yesu, Mfalme. Wale wanaoweka tumaini lao katika kitu kingine chochote kando na Yesu watajikuta wametenganishwa milele na Mungu mwenye upendo ambaye alimtoa Mwanawe wa pekee ili kutuweka huru kutoka katika utumwa wa dhambi. Utengano huu wenye uchungu unaitwa Kuzimu.

Waefeso 2:8–9 Yohana 3:16

jibu

Mungu anakualika kuwa sehemu ya hadithi anayoandika katika enzi zote zijazo. Anatoa wokovu kwako leo, ambao ni mwaliko wako kwa wokovu ambao Mungu hutoa. Unaweza kukubali wokovu wa Mungu kwa:

  • Kukiri hitaji lako kwa Mungu
  • Mwombe akusamehe
  • Kumwamini Yesu pekee akuokoe
  • Kumfuata Yesu Kristo, Mfalme wa maisha yako, kwa imani kuanzia leo

Punde unapomwamini Yesu Kristo, unakuwa MTOTO wa Mungu na Roho Wake anaanza KUISHI ndani yako. Umekuwa sehemu ya hadithi Yake. Kadiri unavyokua katika uhusiano wako na Mungu, ndivyo utakavyoanza kuona na kuelewa hadithi Yake katika maisha yako. Dhambi zako zote, za wakati uliopita na ujao, zimesamehewa, na sasa unapata kibali kamili mbele Zake. Unapoanza uhusiano huu, Yesu anaahidi kuwa nawe katika PANDASHUKA ZA MAISHA na katika furaha na magumu ya maisha haya. Anakupenda kwa upendo wa MILELE, usiobadilika. Na hajaahidi uzima wa milele tu, bali alikuja ili pia upate kujionea kusudi, utimilifu, na uhuru katika maisha haya.

Yohana 6:47

jibu

Mungu anakualika kuwa sehemu ya hadithi anayoandika katika enzi zote zijazo. Anatoa wokovu kwako leo, ambao ni mwaliko wako kwa wokovu ambao Mungu hutoa. Unaweza kukubali wokovu wa Mungu kwa:

  • Kukiri hitaji lako kwa Mungu
  • Mwombe akusamehe
  • Kumwamini Yesu pekee akuokoe
  • Kumfuata Yesu Kristo, Mfalme wa maisha yako, kwa imani kuanzia leo
Ndiyo, Ningependa Kupata Uokoaji!

Punde unapomwamini Yesu Kristo, unakuwa MTOTO wa Mungu na Roho Wake anaanza KUISHI ndani yako. Umekuwa sehemu ya hadithi Yake. Kadiri unavyokua katika uhusiano wako na Mungu, ndivyo utakavyoanza kuona na kuelewa hadithi Yake katika maisha yako. Dhambi zako zote, za wakati uliopita na ujao, zimesamehewa, na sasa unapata kibali kamili mbele Zake. Unapoanza uhusiano huu, Yesu anaahidi kuwa nawe katika PANDASHUKA ZA MAISHA na katika furaha na magumu ya maisha haya. Anakupenda kwa upendo wa MILELE, usiobadilika. Na hajaahidi uzima wa milele tu, bali alikuja ili pia upate kujionea kusudi, utimilifu, na uhuru katika maisha haya.